26 Mei 2015

Tuzo ya BBC:Heko kwa Asisat Oshoala

Mshindi wa Tuzo ya BBC ya mwanasoka Bora wa kike,Asisat Oshoala
Mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Wanawake ya Liverpool, Asisat Oshoala ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa
mwaka.
Oshoala, mwenye umri wa miaka 20 ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo mpya kutoka BBC World Service,kwa kura zilizopigwa na wapenzi wa kandanda duniani.
Mwanadada huyu amemuangusha Veronica Boquete wa Uhispania na Nadine Kessler wa Ujerumani,Scot Kim Little na Marta wa Brazil.
"ninapenda kutoa shukrani zangu kwa BBC,mashabiki wangu duniani na kila mmoja aliyepiga kura" alisema.
Tuzo hii ni ya kwanza kufanyika na Shirika la utangazaji la kimataifa.
Oshoala, ambaye ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wapinzani wake, alikuwa mfungaji bora na alipigiwa kura wakati wa michuano ya kombe la dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20 nchini Canada kipindi cha majira ya joto kilichopita.
Jitihada zake ziliifikisha Nigeria katika hatua ya Fainali ambapo ilikutana na Ujerumani, ambapo Ujerumani ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Nigeria.
Pia alitoa mchango mkubwa katika timu ya wanawake ya Nigeria katika kutwaa ushindi wa kombe la mabingwa Afrika kwa wanawake mwezi Oktoba.
Hatua hiyo imeiwezesha Nigeria kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa wanawake nchini Canada inayoanza tarehe 6 mwezi Juni

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728