Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba anaihama klabu hiyo kwa mara ya pili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 2004 na amefunga mabao 164 katika mechi 381.
Ningependa kucheza tena kwa msimu mmoja zaidi na kwa hilo kufanikiwa itabidi nihamie kilabu nyengine aliuambia mtandao wa Chelsea.
Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho alimsajili kwa mara ya pili Drogba kwa kandarasi ya mwaka mmoja baada ya kuondoka Galatasaray.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni