Burundi imemkataa mwanadiplomasia wa pili aliyeteuliwa na Umoja wa
Mataifa kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.Chama tawala kimesema msuluhishi,Abdoulaye Bathily aliyeteuliwa mwezi uliopita anaegemea upande mmoja.
Hatua hii imefuatia Ripoti ya Umoja wa mataifa kuwa uchaguzi wa ubunge uliofanyika juma lililopita ulitawaliwa na vitendo vya vurugu, kuzuiwa kwa vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao na kukamatwa kwa watu kiholela.
Mpatanishi wa awali, Said Djinit aliachia ngazi baada ya kukosolewa na upinzani uliodai kuwa anapendelea upande wa Serikali.
Burundi imeingia katika vurugu za kisiasa tangu mwezi Aprili, Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania tena nafasi hiyo kwa awamu ya tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni