TASNIA ya filamu imezidi kukua na kusonga mbele kila siku, thamani ya wasanii wanalipwa fedha nyingi kwa kushiriki filamu moja jambo linalomfanya mtayarishaji kutumia wasanii wachache kwa
filamu yake lake katika sinema ya WAKE UP imevunja rekodi kuwashirikisha nyota wengi.
Akiongea na waandishi wa Habari mtayarishaji wa filamu hiyo Manaiki Sanga amesema kuwa sinema hiyo ilikuwa na kazi kubwa kwani hata kama mwigizaji angetaka kuigiza bure shughuli ilikuwa kuwahudumia mahitaji yao kwani ni mastaa wenye mahitaji makubwa katika maisha yao.
“Nashukru Mungu kwa kuniwezesha kufikia ndoto zangu kila siku nilikuwa natamani kufanya kitu cha kipekee katika tasnia ya filamu na nimeweza kuwashirikisha wasanii nyota wote ,”
“Nimetumia fedha nyingi sana lakini lengo ni kuwa tofauti na wenzangu katika utayarishaji ilikuwa ni kazi ngumu katika kuwapata na kuwashirikisha, namshukru sana Lamata Director wangu,”anasema Manaiki.
Filamu hiyo ambayo ipo tayari inatarajia kutoka mwezi wa nane mwaka huu imewashirikisha wasanii kama Kajala Masanja, Amri Athuman ‘King Majuto’, Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Tausi Mdegela, Yusuf Mlela, Manaiki Sanga, Chuchu Hans, Mutrah, Asha Boko na nyota wanaofanya vizuri katika filamu Bongo Movie.
Sinema hiyo ambayo inaleta mapinduzi katika tasnia ya filamu Bongo itasambazwa na kampuni ya usambazaji wa filamu za kibongo ya Steps Entertainment nchi nzima na kuona jinsi wasanii walivyoshindana humo na kuinogesha filamu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni