Chile imewashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na kushinda kombe kubwa zaidi kati ya nchi za Marekani ya
kusini la Copa Amerika.
Hili ndilo kombe la kwanza la kimataifa kuwahi kushindwa na Chile.
Chile ambayo ni waandalizi waliwashinda Argentina mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukosa kufunga.
Ni miaka 22 tangu Argentina washinde kombe lolote kubwa kwenye mashindano ya kandanda ya kimataifa.
Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever Banega ukinyakwa na kipa Claudio Bravo.
Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo.
Sanchez karibia afunge katika dakika za ziada.
Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliojaa kuishabikia timu yao ni wachimba mgodi 33 waliokwama chini ya mgodi kwa wiki kadhaa mwaka 2010,katika kisa kilichovutia hisia nyingi duniani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni