02 Julai 2015

Nuhu Mziwanda: Sipo na Shilole Hivi Sasa

Nuhu Mziwanda: Sipo na Shilole Hivi SasaMsaniii Nuhu Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya 'Bilima' amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hayupo na Shilole, Nuhu amesema hayo jana alipokuwa Kikaangoni akichat na mashabiki kupitia ukurasa wa facebook wa EATV.


Toka ulipoaanza mwezi wa ramadhan kulikuwa na tetesi kuwa msanii Nuhu amehama kutoka kwa Shilole na sasa anaishi kwake mwenywe hilo limethibitishwa Nuhu alipokuwa akijibu swali la kwanini mpaka sasa anaendelea kuishi na Shilole kwenye nyumba ambayo Shilole amepanga.

"Hapana sipo na Shilole kwa sasa mimi nipo kwangu"

Lakini kauli ya Nuhu haina maana kuwa mapenzi yao yamekufa lahasha bali amempisha mwenzake katika kipindi cha mfungo wa ramadhan kutokana na misingi ya imani ya mpenzi wake na kudai kuwa licha ya hilo hivi sasa yeye mwenyewe anakwake na anamaisha yake mwenyewe.

Maswali mengi ambayo mashabiki wa ukurasa wa EATV walikuwa wakiyauliza yalikuwa ni kuhusu maisha ya mapenzi kati yake na Shilole hivyo walikuwa wakihitaji kufahamu mambo mbalimbali ambayo huenda wanaona kama yanazushwa na jamii hivyo ilikuwa ni sehemu ya wao kupata ukweli, mashabiki wengi walikuwa wakiiuliza inakuaje anakubali kupigwa pigwa na mwanamke kama mtoto na hapo ndio Nuhu Mziwanda alipoweka wazi suala hilo la yeye kupewa kichapo na Shilole.

"Hamna mapenz bila kugombana na siku zote ukitaka kudumu na mwanamke usimuonyeshe ubabe sababu mwanaume wa kweli hapigi na hata kama ukipigwa kibao na mwanamke hauwezi kufa hivyo ni vema kua kama mwanaume na kusamehe"

Mbali ni hilo Hit maker huyo wa Bilima alikana suala la yeye kulelewa na Shilole na kusema kuwa yeye ana maisha yake na mpenzi wake huyo ana maisha yake pia hivyo halelewi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyosema mitaani kuwa analelewa na kutunzwa na Shilole.

"si kweli mimi silelewi maana nina maisha yangu na shishi ana maisha yake so tumekutana tu kimapenzi ila watu wanajudge tofauti ila wanapaswa kutambua kuwa mimi na maisha yangu na Shishi pia ana maisha yake binafsi,ni mapenzi tu yanafanya kuwa kitu kimoja"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728