Brenda Myers-Powell alikua mtoto wakati alipoanza kufanya ukahaba katika miaka ya sabini. Alizaliwa eneo la Chicago, Marekani na mamake mzazi alifariki dunia akiwa na miezi sita pakee.
Hapo ilimlazimu kusalia na bibi yake. Aligundua baadaye kwamba mamake alikufa kutokana na ulevi wa kupindukia.Kwa sababu bibi yake alikua mfanyikazi wa ndani ilimlazimu Brenda kujipeleka shule na kurejea nyumbani wenyewe licha ya kwamba alikua kwenye chekechea.
Baadhi ya watu walimdhulumu kingono mtoto huyo wakati alipokua akitoka chekechea.
Mwanamama huyu alifanya ukahaba kwa miaka 15, wakati huu wote hakuwahi kujiingiza katika mihadarati. Lakini kutokana na mazingira magumu kwenye madanguro ya ukahaba, hakuwa na budi kuanza kutumia mihadarati ili kusahau maisha aliyokua akiishi.
Baadaya ya miaka 25 kama kahaba, siku moja alikutana na mteja ambaye alikua katili.Alimtupa nje ya gari lake huku likienda kwa muendo wa kasi. Brenda alipata majeraha mabaya kiasi cha kupelekwa hospitalini akiwa mahututi.
Lakini madaktari waliokua wakimhudumia walimdhihaki kwamba alipata alichotaka na kumsuta kwamba alikua kahadaa mteja ndiposa akapata adhabu. Hapo wakawaita polisi kumkamata.
Lakini kwa bahati nzuri daktari mmoja alizungumza na Brenda na kumshauri afike katika kituo cha huduma ya jamii maarufu kama Genesis House. Msimamizi wa kituo hiki alikua Bi Edwina Gateley raia wa Uingereza.
Ni katika kituo cha Genesis Brenda alipata maisha mapya na kuanza safari ya kupona machungu, adhabu na kero za ukahaba. Hakupata shinikizo za kuondoka hadi pale alipohakikisha maisha yake yalikua shwari.
Kwa sasa Brenda anawasaidia wanawake na wasichana wanaokimbia ukahaba. Aidha alijaaliwa kuwa na familia, mume na wanawe wawili wa kike. Ana pia wajukuu. Maisha yake ni kuwafundisha soka watoto na kuhakikisha wanaishi kwa maadili mema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni