Seifeddine Rezgui, mshambuliaji wa Tunisia aliyewaua watu 38 katika mgahawa wa kifahari eneo la Sousse anaaminika kupata mafunzo ya vita nchini Libya.
Wizara ya ndani imesema kwamba Rezgui amekuwa nchini Libya tangu mwezi Januari sawa na wanaume wawili walioshambulia makavazi mjini Tripoli mwezi Machi. Wengi waliouawa kwenye shambulio la Sousse ni watalii wakiwemo Waingereza 30.
Kundi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulio hilo.Rezgui alipata mafunzo ya itikadi kali wakati akisomea shahada ya uhandisi.
Tayari maafisa wa Tunisia wamewakamata washukiwa kadhaa wanaodaiwa kushirikiana na mshambuliaji huyo. Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi amekiri kwamba maafisa wa usalama hawakutarajia shambulio kama hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni