Mmoja wa viongozi katika mapinduzi yaliyozimwa nchini Burundi hivi karibuni ya kumpindua Rais Piere Nkurunziza ameiambia BBC kuwa waasi wao wamekuwa wakiwapa mafunzo polisi na
askari kwa ajili ya jaribio jingine la kumwondoa rais Pierre Nkurunziza.
Akiwa uhamishoni Generali Leornard Ngenda Kumana amekanusha kuwa walisaidia na mataifa ya nje.
Wamekuwa wakimshutumu Rais Nkurunziza kuwa kusababisha vurugu kaati ya jamii ya wahutu na watutsi na kuwapa silaha wapiginaji wa vijana waoiunga mkono serikali ambao wanaonekana wengi ni kutoka jamii ya wahutu.
Zaidi ya watu laki moja wamekimbia nchi hiyo wakihofia vurugu wakati wa uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Wanaompinga wanasema hatua ya kugombea urais kwa muhula wa tatu kwa rais huyo ni kinyume cha katiba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni