Familia moja ya watu 12 nchini Uingereza ambayo ilitoweka imejiunga na kundi la wapiganaji wa IS na
kwamba iko salama salmin,kulingana na taarifa iliotumwa kwa niaba yao.
Taarifa hiyo inayodaiwa kutumwa na mwanachama mmoja wa wapiganaji hao imesema kuwa inashangazwa kusema kuwa familia hiyo ilitekwanyara na kulazimishwa kujiunga na kundi la IS imewataka waislamu wote kujiunga na kundi hilo ili kumtii Allah.
Familia hiyo kutoka Luton haijaonekana tangu mwezi May tarehe 17 na inashirikisha watoto watatu walio na umri wa kati ya mwaka 1 na 11.
Maafisa wa polisi hapo awali walisema kuwa huenda familia hiyo ilikwenda Syria.
BBC haijathibitisha iwapo taarifa hiyo iliyo na picha mbili za mmoja ya watu wa familia hiyo Muhammed Abdul Mannan ni ya kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni