Viongozi wawili wa kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Al shabaab nchini Somalia wameuawa kwenye shambulio la mabomu ya angani.
Watu katika mji wa Baardhere ulioko kusini mwa nchi hiyo wanasema walisikia milipuko asubuhi ya leo katika eneo hilo.
Kisha wapiganaji hao wa Al shabaab wakafika eneo hilo la tukio.
Baardheere ni moja ya miji ambayo bado ingali inadhibitiwa na wapiganaji wa Al shabaab.
Wanajeshi wa muungano wa Afrika na wale wa serikali ya Somalia wanakaribia eneo hilo.
Viongozi kadhaa wa kundi hilo wameuawa kwenye mashambulio ya mabomu ya angani yaliyoangushwa na wanajeshi wa Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni