Ndege inayotumia umeme wa jua imetua mjini Hawaii baada ya kuweka historia ya kuruka kilomita 7,200 katika eneo la pacific kutoka Japan.
Rubani Andre Borschberg aliishusha ndege hiyo polepole katika uwanja wa ndege wa Kalaeloa.
Umbali na saa ambayo ndege hiyo ilichukua hewani ni saa 118.
Mda huo pia ni rekodi ya ndege ambayo haitumii mafuta.
Mda huo uliowekwa na bwana Borschberg umeboreshwa zaidi ikilinganishwa na ule uliowekwa na Steve Fossett aliyetumia saa 76 katika ndege ya mtu mmoja mwaka 2006.
Licha ya kukaa katika kiti cha nahodha kwa mda mrefu,nahodha huyo wa Uswizi aliiambia BBC kwamba hakusikia uchovu.
''Tuliungwa mkono na watu wengi wakati wa safari yetu na hilo lilinipatia motisha'',alisema .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni