06 Julai 2015

Ugiriki wapiga kura ya Hapana

Raia wa Ugiriki wakifurahia matokeo ya kura ya hapana.
Maelfu ya raia wa Ugirik usiku wa leo wametawanyika katika mitaa ya mjini Anthens karibu na jengo la bunge, wakifurahia kura ya hapana waliyoipiga ambayo imeshinda kwa
ya asilimia 60.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras,amesema matokeo hayo ya hapana, hayana nia ya kwenda kinyume na jumuiya ya Ulaya bali yataiongezea Ugiriki uwezo wa majadiliano zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni.
Tsipras ameongeza kuwa serikali ya Ugiriki iliitisha kura hiyo ya maoni ikiamini kuwa kura ya Hapana italeta makubaliano mazuri, pamoja na kwamba kuna onyo kutoka kwa viongozi wa ukanda wa Euro kuwa hatua hiyo itasababisha Ugiriki kuondolewa katika nchi wananchama wa ukanda huo.
Naye Rais wa Bunge la Jumuiya ya Ulaya Martin Schulz amesema kuwa kura hiyo ya HAPANA inaiacha Ugiriki katika mazingira mabaya zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni na vikwazo vya kimataifa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anasema kwa matokeo hayo sasa umamuzi ni wa mahakama ya Ugiriki kwani wapiga kura wamepinga kwa nguvu zote masharti ya wakopeshaji wa kimataifa
Matokeo haya yanasababisha kukubalika zaidi kwa Waziri mkuu wa Ugirik Alexis Tsipras japo kuwa pia anakuwa na wajibu mkubwa wa kukabiliana na mazingira yote ya kipindi hiki cha mpito kuhusiana na mzozo wa madeni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728