Onyo: Ukikojoa kwenye ukuta wowote wa mji wa San Francisco , huenda mkojo ukakurudia
Ajenti wa wizara ya nguvu kazi mjini humo amesema kuwa wanajaribu aina ya rangi ya ukuta inayorudisha mkojo katika maeneo ambayo ni maarufu kwa watu kujisaidia ovyo ovyo.
Mtu yeyote atakaye tumia ukuta uliopakwa rangi hiyo, mkojo wao utawarudia, hiyo ni kulinganana na msemaji wa mawakala hao.
Mkurugenzi wa mawakala hao alipata wazo hilo baada ya kupata maarifa kuhusu rangi hiyo akiwa katika sehemu moja ya burudani nchini Ujerumani.
Kundi la Jamii ya eneo la Hamburg's IG St Pauli lililazimika kutumia rangi hiyo ili kukabiliana na shida iliyosababishwa na watalii millioni 20 wanao zuru wilaya hiyo kila mwaka.
Na ilipofikia mwezi Machi , walikiambia kipindi cha BBC news beat kwamba rangi hiyo inaonekana kufaulu na shida hiyo hatimaye imepata suluhu.
Rangi hiyo inayojulikana kama Ultra-Ever Dry inatengeza kizuizi cha hewa mbele ya ukuta huo ambao utafanya mkojo na aina yoyote ya maji kugonga na kurudi, hii ni kulingana na watengezaji wa rangi hiyo.
Katika majaribio ya mradi huo, mamlaka ya San Francisco ilipaka rangi kuta 9 zilizo karibu na maeneo ya burudani na makaazi ya watu wasio na nyumba.
Maandishi yaliondikwa kwa lugha ya kiingereza, kichina na kihispania kwenye kuta hizo yalisema, shikilia kwanza , tafuta usaidizi mahali pengine.
Fikra hiyo ni kuwafanya watu wafikirie mara mbili kabla ya kukojoa hadharani, alisema Rachael Gordon msemaji wa idara ya nguvu kazi.
Tumepata simu nyingi kutoka kwa watu wanaotaka wapakiwe rangi hizo kwenye majengo yao maeneo jirani, Alisema Gordon.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni