Msanii Shilole Kiuno alimaarufu kama Shishi Baby amepata bahati ya kuzindua msimu mpya wa kipindi cha Mkasi TV ambacho kinarushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa tatu na nusu usiku kupitia Televisheni namba moja kwa vijana EATV.
Mkasi TV inarejea tena kwa kasi kubwa baada ya kufanyiwa mabadiliko na kuboreshwa zaidi ili kuleta hamasa na kuzidi kuwahamasisha watazamaji kuendelea kuwa katika familia hiyo inayokuwa kila siku, muonekano mpya wa mkasi TV hautafanana na ule wa awali.
Shilole alikutana na watangazaji wa Mkasi TV, Salama, Mubah na John na hapo ndipo alipoweza kufunguka mambo mengi kuhusu maisha yake na muziki kiujumla, kama ambavyo unafahamu Salama, Mubah na John wanapokutana na mtu mwenye skendo na mambo mengi ya kuzungumza lazima atafunguka, hivyo fanya uwezavyo Jumatatu utazame mabadiliko ya kipindi hicho huku Shilole akifunguka mambvo mengi.
EATV.TV
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni