Aliyewahi kuwa swahiba wa mbunge mtarajiwa Wema Sepetu, Snura Mushi ametoa kauli zenye mlengo wa kumpiga vijembe Wema.
“ Naepukana na unafiki tena naweza kusema ni roho mbaya chuki kwa baadhi ya wasanii kuunda makundi ambayo yanatumia muda mwingi kuwadis wengine, mfano hivi sasa wakati Diamond anawania tuzo za kimataifa eti kuna watu wanaungana na watu wan je kufanya kampeni ashindwe,” alisema Snura.
Snura anadai kuwa siku hizi makundi ambayo yanaundwa na wasanii au wapenzi wenyewe ambayo yanatumika vibaya katika kutengeneza ugomvi au kushabikia wasanii wakigombana kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwatusi na kuwakatisha tamaa hata kama wanafanya kazi zinazotangaza Taifa.
Wema Sepetu ni miongozni mwawasanii ambao wanadaiwa kuhamasisha kundi lake “team Wema” kumpigia chepuo msanii wa Nigeria Davido ambaye anachuana na Diamond wa hapa nyumbani katika tuzo za MTV Africa MAMA.
KIU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni