Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea vikwazo ikiwemo marufuku ya usafiri na kupiga tanji mali za majenerali sita wa Sudan Kusini.
Watatu ni kutoka upande wa serikali na wengine watatu ni kutoka upande wa waasi.
Hatua hii inajiri siku chache baada ya ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuonyesha ukatili mkubwa wa kibinadamu katika mapigano yanayoendelea nchini humo.
Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power amesema vikwazo hivyo ni onyo kwa wale wanaendeleza ukiukaji wa kibinadamu Sudan Kusini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni