Msanii wa muziki aina ya rap Sean P Diddy Combs amesema kuwa hatakabiliwa na mashtaka ya
shambulio kufuatia kisa kimoja mwezi uliopita kilichohusisha uzani wa 'kettlebell'.
P Diddy aliye na umri wa miaka 45 alikamatwa mnamo Juni 22 kwa tuhuma za kushambulia kwa kutumia silaha hatari katika chuo kikuu cha California.
Alizuiliwa katika jela kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya dola 160,000.
Hakimu wa wilaya hiyo ameipeleka kesi hiyo katika mji wa Los Angeles kuamua iwapo Combs atakabiliwa na mashtaka hafifu.
''Tunafurahia kwamba hakimu alikataa mashtaka ya kutumia nguvu kupitia kiasi dhidi ya Combs'',alisema wakili wake.
Vyombo vya habari vilisema kuwa P Diddy alihusika katika mgogoro kati yake na kocha wa timu ya soka ya Marekani chuoni humo.
Hatahivyo Combs amesema kuwa alikuwa akimtetea mwanawe Justin Combs ambaye ni mchezaji wa timu ya chuo hicho na kwamba alikuwa akifanya mazoezi wakati wa tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni