China imewaonya raia wake wanaosafiri kuelekea Uturuki kutoshiriki maandamano ya kuipinga Beijing.
Waziri wa mambo ya nje anasema watlii kadhaa wa China wameshambuliwa. Ushauri huo umetolewa wakati hofu inaongezeka kati ya nchi hizo mbili kuhusu namna China inavyowachukulia waislamu wa Uighurs katika eneo lake huko magharibi- Xinjiang. Mwishoni mwa juma, mamia ya waandamanaji wamekusanyika nje ya ubalozi wa China katika mji mkuu wa Istanbul wakiishutumu Beijing.
Ni ishara ya hivi karibuni ya kuongezeka kwa hisia dhidi ya China nchini Uturuki. Ankara imemuita balozi wa China nchini humo wiki iliyopita kufuatia taarifa kwamba Beijing imewapiga waislamu wa Uighurs marufuku kufunga na kuabudu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. China imejibu kwa kusema inalinda uhuru wa kuabudu.
Hatua hiyo ya Beijing kwa waumini hao wa Uighurs ni sula muhimu kwa Waturuki wengi kwasababu wana uhusiano wa karibu wa kitamaduni na kidini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni