Wabunge nchini Uingereza wametakiwa kufikiria kuiruhusu Uingereza kushambulia maeneo ya wapiganaji wa Kiislam wa Islamic State nchini Syria, anasema waziri wa
ulinzi wa Uingereza, Michael Fallon.
Jeshi la Uingereza,RAF limekuwa likifanya mashambulio nchini Iraq tangu mwezi Septemba lakini Bwana Michael Fallon anatarajiwa kuliambia bunge kuangalia uwezekano wa kupeleka pia majeshi yake nchini Syria.
Bwana Fallon anasema hakuna kikwazo kisheria lakini amewahakikishia wabunge kwamba hakuna uamuzi utakaochukuliwa bila ruhusa yao.
Katika hotuba yake Bwana Fallon atazungumzia mashambulio ya kigaidi, kama mauaji ya Tunisia, huenda yalipangwa na wapiganaji wa IS nchini Syria.
Watalii 29 kati ya 38 waliouawa katika pwani ya Sousse nchini Tunisia tarehe 26 Juni wamethibitika kuwa raia wa Uingereza.Mwanafunzi Seifeddine Rezgui, mwenye umri wa miaka 23, aliuawa kwa kupigwa risasi baada kufanya shambulio hilo.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema IS bado ni kitisho kwa nchi za magharibi na washirika wake katika nchi za Iraq na Syria walikuwa wanapanga mashambulio ya kutisha katika ardhi ya Uingereza.
Miili ya baadhi ya Waingereza waliouawa kwa kupigwa risasi katika shambulio la fukwe za Tunisia imewasili nchini Uingereza. Waziri mkuu alishindwa katika bunge miaka miwili iliyopita, wkati wabunge wa chama cha Labour walipoungana kupinga mashambulio ya anga katika maeneo yaliyokuwa yakishambuliwa na serikali ya Syria ili kuzuia matumizi ya silaha za kemikali ambazo zilihofiwa kutumiwa na serikali hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni