Jeshi la Uganda linasema kuwa kiongozi wa kundi la waasi linalolaumiwa kwa mauaji ya karibu watu 1000 amekabidhibiwa Uganda baada ya
kusafirishwa kutoka nchini Tanzania.
Jamil Mukulu ambaye alikamatwa nchini Tanzania mwezi Aprili, ni kiongozi wa kundi la ADF ambalo limelaumiwa kwa kuendesha mashambulizi mashariki mwa Uganda na mji mkuu Kampala.
Pia anatakikana kwa mashtaka yanayohusiana na vita nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Jeshi la Congo liliendesha oparesheni kubwa dhidi ya waasi wa ADF mwaka uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni