Mkazi wa Busoka wilayani Kahama Mulele Ramadhan (19) ambaye alikuwa dereva wa bodaboda ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumbuni na mtu asiyefahamika aliyekuwa na nia ya kumpora pikipiki.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 7 mchana katika barabara inayoelekea Kitwana ambapo marehemu alikodiwa na mtu asiyefahamika katika kituo cha pikipiki kilichopo mtaa wa Manzese na walipofika njiani mtu huyo alitekeleza mauaji hayo.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia kahama fm kuwa wakati wa tukio hilo marehemu alipiga kelele za kuomba msaada na ndipo watu walipojitokeza kumpa msaada, lakini muuaji huyo akatokomea kusiko julikana.
Mganga mkuu wa hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama Dk. Bruno Minja amethibitisha kumpokea Mulele akiwa majeruhi, lakini akifariki dunia majira ya saa 9 alasiri wakati wakiwa katika harakati za kuokoa maisha yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justius Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa omba wananchi wa eneo hilo kutoa ushirikiano kwa polisi ili kuweza kumkamata mtu huyo ambaye ametekeleza mauajia hayo.
Mwili wa marehemu Mulele umehifadhiwa kwenye chimba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama, huku ukisubiri taratibu za mazishi kutoka kwa ndugu wa marehemu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni