28 Julai 2015

Lowassa akihama chama cha CCM

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa leo amejiunga rasmi na Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA na kuondoa hali ya
sintofahamu miongoni mwa watanzania baada ya kutopata nafasi ya kuteuliwa na Chama cha mapinduzi ,CCM kupeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.
Akizungumza katika Mkutano uliowakusanya wanachama waliounda UKAWA, na waandishi wa habari, Lowassa alisema amekubali mwaliko wa kujiunga na UKAWA hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Amesema baada ya kutafakari kwa kina baada ya yale yaliyotokea katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM mjini Dodoma kutoridhishwa nayo, ameamua kujiengua na chama hicho.
''Katiba ya CCM ilikiukwa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi,nilifanyiwa mizengwe,majungu na habari za uongo kuhakikisha kuwa jina langu halifikishwi kwenye kamati kuu na halmashauri kuu kwa ajili ya kujadiliwa licha ya kuwa nilikuwa nikiungwa mkono na Wanachama wengi zaidi kuliko wagombea wengine'' alisema Lowassa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728