Mwanamfale wa Saudi Arabia ambaye pia ni bwenyenye Alwaleed Bin Talal amesema kwamba atatoa mali yake yote ya kima cha dola bilioni 32 kwa shirika la
hisani.
Mwanamfalme Alwaleed wa miaka 60 ni miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani. Amesema kwamba amependezwa sana na wakfu wa Bill na Melinda Gates ulioanzishwa mwaka wa 1997.
Anashikilia nafasi ya 34 katika orodha ya Forbes ya matajiri wakubwa duniani. Hana wadhifa wowote katika serikali ya Saudi Arabia lakini ni mwenyekiti wa kampuni ya uwekezaji ya Kingdom Holding Company.
Kampuni hii ina hisa katika hoteli kubwa The Four Seasons. Fairmount na Raffles. Pia inaumiliki katika kampuni ya News Corp, Benki ya Citigroup, Twitter na Apple.
Mwanamfalme atatoa utajiri wake binafsi kando na umiliki wake katika kampuni ya Kingdom Holding.
Ameongeza msada huu utasaidia kuimarisha uelewa wa utamaduni tofauti, ustawi wa jamii, kuboresha maisha ya wanawake na kuwezesha vijana kuchangia masuala ya dharura pamoja na kuendeleza jamii inayovumiliana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni