Chelsea imemsajili mshambuliaji wa klabu ya Monaco Radamel Falcao kwa makubaliano ya mkopo lakini kuna uwezekano wa kuongeza kandarasi hiyo na kuwa ya kudumu.
Falcao mwenye umri wa miaka 29 alicheza kama mchezaji wa mkopo katika kilabu ya Manchester United na kufanikiwa kufunga mabao manne katika mechi 29.
Anakutana na wachezaji wenza wa zamani katika kilabu ya Athletico Thibaut Courtois,Filipe Luis na Diego Costa.
Mchezaji wa Croatia Mario Palic mwenye umri wa miaka 20 naye ataelekea Monaco Kucheza kwa mkopo.
Falcao alisema kuwa anafurahia kuichezea Chelsea.
''Natamani kuanza kufanya mazoezi kwa lengo la kuisadia timu yetu kulidhibiti taji la ligi kuu pamoja na kupata ufanisi Ulaya''.alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni