02 Julai 2015

Ghadhabu baada ya wauaji kuachiwa huru

Mwanamama Farkhunda
Farkhunda alipigwa mawe kwa kisingizio kwamba aliiteketeza Koran
Makundi ya kutetea maslahi ya wanawake yameghadhabishwa na mahakama ya rufaa nchini Afghanistan ambapo
imebatilisha hukumu ya kifo dhidi ya wanaume wanne waliohusika na mauaji ya mwanamke mjini Kabul mwezi Machi.
Wakili wa familia ya mwanamke huyo amelalamikia mahakama hiyo kwa kuendesha uwamuzi wake faraghani. Naye kakake marehemu amesema uwamuzi huo ni ukiukaji mkubwa wa haki.
null
Wanaume wanne walikua miongoni mwa waliompiga mawe hadi kufa Farkhunda
Mwanamke huyo kwa jina Farkhunda, alishambuliwa katika msikiti mmoja baada ya kutuhumiwa bila ukweli kwamba aliiteketeza Koran. Alipigwa mawe hadi kufa, maiti yake ikakanyagwa kwa gari na kisha ikateketezwa.
Mahakama ya rufaa pia imemuachia huru msimamizi wa msikiti huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728