Mashabiki wa manchester United wengi walijua kuwa Van Persie anaondoka kuelekea Fenabashe lakini kwa mtoto mdogo mwingereza wa
miaka minne Louis Diamond hakufahamu kuwa kipenzi chake Robin Van Persie anaondoka mpaka pale alipoambiwa na wazazi wake kwamba mpachika magoli Robin alikuwa tayari kuelekea uturuki. Hivi sasa waturuki wameanzisha kampeni ya kuchangishana pesa ili mtoto huyo ambaye video yake imesambaa mitandaoni na kutizamwa na watu wengi aletwe Uturuki kumshuhudia mchezaji huyo.
Shabiki huyo mdogo wa miaka minne alipoambiwa na wazazi wake kuwa Van Persie alirekodiwa na baba yake akilia sana na video yake imesambaa mitandaoni duniani kote.
"hatujamwambia kama video yake imesambaa duniani, tumemwambia tu kuwa tumewaonyesha marafiki zake tu hapa mtaani tu hajui kama ni dunia nzima, mimi na mke wangu tuna hamu ya kumwona atakavyocheka tukimwonyesha video hii miaka kumi baadaye" Alisema baba wa mtoto huyo.
Kuna uwezekano pesa iliyopangwa kuchangwa mashabiki wa uturuki ikazidi kiwango cha pauni 1200 za uingereza kilichokusudiwa kumsafirisha mtoto huyo na baba yake ili kuja kushuhudia mechi ya kwanza ya Van Persie nchini uturuki.
Ni vema pia mtoto akapozwa kwa kuambiwa kuwa kinakuja chuma kipya kutoka southampton, Morgan Shineidelini ambaye atafanya vipimo Man U.
Kwa upande mwingine Liverpool inachukua kitita cha pauni milioni 49 kumuuza Raheem Sterlin kuelekea Man City na kumfanya kijana huyo mdogo wa miaka 20 kuwa mchezaji wa ghali zaidi katika england.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni