02 Mei 2015

Wolper Anaswa na Kigogo Mpya

Wolper Anaswa na Kigogo Mpya!Achilia mbali akina pedeshee Mangi, Dallas na Gee Modal, kigogo mpya wa staa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe safari hii amenaswa laivu wakijiachia kwa raha zao, Risasi Jumamosi lina cha kushika mkononi.

Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la risasi la leo, kigogo huyo ni mtu mwenye fedha zake aitwaye Jimmy Mgaya ambaye ni Mbongo mfanyabiashara aishie nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Chanzo hicho kilishusha data kuwa jamaa huyo ndiye aliyempangia Wolper nyumba ya kifahari iliyopo ushuani Mbezi-Beach jijini Dar.Huku akirusha picha za kimahaba za wawili hao, sosi wetu huyo alisema kuwa Jimmy ni ‘mtu f’lani hivi amazing’ kwa sababu anakata mkwanja kinoma.
“Kama mtakumbuka kuna siku gazeti lenu mliandika kuwa Wema (Sepetu) na Wolper walilewa chakari kwenye pati ya ‘bethidei’ ya Petit Man, basi huyo kigogo ndiye aliyewafanyia kufuru na ile pati ilifanyika nyumbani kwake, Kinondoni-Manyanya (Dar),” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.
Chanzo hicho kilidai kwamba picha za wawili hao wakijiachia ambazo gazeti hili linazishikilia zilipigwa maskani kwa jamaa huyo huko Durban kwenye Jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, gazeti hilo lilimtwangia simu Wolper na kumsomea mashitaka yake juu ya mwanaume huyo ambapo mbali na kukiri kumfahamu Jimmy, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli namfahamu Jimmy, nilikutana naye kwenye mizunguko yangu nje ya nchi. Si kweli kwamba ni bwana’ngu. Kuhusu picha, nilipiga naye kama rafiki tu na sioni kama ni picha mbaya.”
Hivi karibuni Wolper alikiri kuwa na mwanaume lakini akawa anaogopa kumwanika kwa kuogopa kuporwa na wasichana wa mjini hivyo inaaminika ndiye huyo Jimmy.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728