ANGA wamefikiria kikosi chao wakaanza kukuna kichwa na kufikiria kwamba inaweza kutokea kasheshe kubwa kama mawinga wawili, Simon Msuva na Mrisho Ngassa watakosekana Jangwani msimu ujao.
Wachezaji hao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho hususani msimu huu ambao Msuva licha ya kutengeneza mabao mengi kama ilivyo kwa Ngassa, amekuwa mfungaji bora kwa mabao yake 17. Ngassa mwenye mabao manne tayari ameshasaini mkataba na klabu ya Free State ya Afrika Kusini wakati Msuva amefuzu majaribio Bidvest Wits ya hukohuko na kinachosubiriwa sasa ni ofa yake kuletwa rasmi Yanga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni