07 Mei 2015

Saa za Apple zakosolewa

Saa za Apple aina ya Smart watch
Kampuni ya Apple imekiri kwamba 'tattoo' za kifundo cha mkononi zinaweza kuathiri uangalizi wa moyo wa binaadamu katika saa za
kampuni hiyo ,siku chache tu baada ya malalamishi kutoka kwa watu walio na 'tatoo' kwamba saa hizo aina ya Smartwatch haziweza kusema iwapo wako hai ama la.
Tatizo hilo limezuka kwa sababu saa hiyo hutumia miale ya rangi ya kijani inayong'ara ndani ya ngozi ili kubaini kiwango cha moyo unavyopiga.
Lakini kwa watu walio na 'tattoo' katika kifundo cha mkono ,wino unaotumika huzuia mwangaza huo wa kijani kibichi na hivyobasi kutoa matokeo mabaya.
saa za Apple
Kampuni ya Apple hatahivyo haijatoa tamko lolote kuhusu habari hiyo lakini imearifu ukurasa wa usaidizi wa saa hiyo kubaini tatizo hilo.
Huku kampuni hiyo ikiwa imeliangazia swala la kiwango cha moyo wa binadaamu unavyopiga,na kusahau kwamba wateja wake wamekuwa wakilalamika kuhusu sensa ya ngozi katika saa hiyo,ambayo inachukua habari za iwapo saa hiyo imevuliwa na inawabidi watumiaji kuweka neno la siri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728