Ubuyu Mpya Kutoka Instagram kwenye page ya mrekebishatabia kuhusu Mrembo
Mwigizaji Wolper Kumsahau aliyemwingiza katika Tasnia ya Filamu:
'HISTORIA: Je unajua aliyemtoa kisanii Jackline Wolper mpaka kupata
umaarufu nchini ni nani? Ni mdada mkali wa wa siku nyingi kwenye masuala
ya sana Lucy Komba ambaye hivi sasa anaishi na familia yake nchini
Denmark.
Alikutana nae kwenye ofisi moja bongo akamuomba namba ya simu
walipoachana baada ya kama dk 10 akamuandikia msg anaomba amsaidie
kwenye sanaa awe kama yeye Lucy Komba , Jackline alikuwa na saloon ya
nywele kipindi hiko baadae saluni ya Jackline Wolper ilifungwa sababu ya
kushindwa kulipa kodi, ikafikia hatua akauza gari yake na akaanza
kutumia gari ya Lucy Komba... anam-drive Lucy kazini anatumia gari jioni
anarudi kumfuata kazini... mambo yakawa magumu kwa Jackie mpaka akauza
vitu vya saluni, wakati huo ndo Lucy kwa bidii anamfundisha jinsi ya
kuigiza...mpaka baba watoto wa Lucy akawa anamuonea huruma Lucy kumtaka
apate muda apumzike!! Haikuishia hapo Lucy akamuunganisha kwenye filamu
akawa anaharibu wadau wanamlaumu Lucy kuwa Jackie atoke maana hajui
lakini akamtetea na kuendelea kumfundisha mpaka akacheza vizuri.
Filamu za Lucy mbili ya kwanza ilikuwa inaitwa AMA ZAKO AMA ZANGU ya
pili KIPENZI CHANGU baada ya hapo Irene Uwoya akampigia simu Lucy
kumuuliza kama ana mtu anataka kufanana naye. Lucy akampigia Jackline na
kumwambia akaonane nae na Kanumba na Ray wakaridhia ndo wakamchezesha
ile scene ya Ophra baada ya hapo akaanza kudai Ray ndo amemtoa kwenye
sanaa kwa ile scene moja aliyocheza.
Lakini baada ya watu kumponda ndo akabadilika na kusema Lucy ndo kamtoa
na mpaka leo ndo kisa cha watu kumfahamu Jackline Wolper.... kuumbe Lucy
ndo kakufikisha hapo @wolperstylish?? Kila mmoja ana mahali alianzia
lkn jaribu kukumbuka Wema hata kama ni kidogo...Halafu jinsi alivyo hata
harusi yake hukuudhuria ukaishia kuiponda!! Watu hawakumbuki walikotoka
aisee'
06 Aprili 2015
Mwigizaji Jack Wolper Ashutumiwa Kumsahau Aliyemtoa Kisanii Katika Tasnia ya Filamu Bongo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni